CCM Arumeru waomboleza kifo cha mfanyabiashara

CCM Arumeru waomboleza kifo cha mfanyabiashara

WAKATI mwili wa mfanyabiashara maarufu wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Itandumi Makere ukitarajiwa kuzikiwa Jumamosi, Machame mkoani Kilimanjaro, Chama cha Mapinduzi wilayani Arumeru, kimetoa pole kufuatia  msiba huo.

Makere ambaye alikuwa mmiliki wa jengo la  Rotterdam, lililopo karibu na kituo cha Polisi Usa-river, ametoa ajira kwa watu mbalimbali, ambapo pia amekuwa mshiriki mkubwa wa shughuli za Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na serikali.

Katibu Mwenezi wa CCM, Wilaya ya Arumeru, Kennedy Mpumilwa amewaongoza baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Meru kutoa pole nyumbani kwa mfanyabiashara huyo eneo la USA -River wilayani Arumeru.

Advertisement

Mfanyabiashara  huyo alifikwa na mauti juzi na anatarajia kuagwa kesho.

Akitoa pole nyumbani kwa mfanyabiashara huyo, Kennedy amesema marehemu alikuwa ni mfanyabiashara na mtu aliyejitoa kwa watu ikiwemo kutoa ajira mbalimbali kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Amesema chama kimepata pigo kutokana na msiba huo, hivyo alitoa pole kwa familia na jamii kwa ujumla kutokana na kifo cha mfanyabiashara Makere.

Wakati huo huo, Mpumilwa amemtembelea kumjulia hali, diwani wa kata ya USA-River, Omary Mshana aliyetenguka mguu.