CCM hatubebwi tumejipanga – Makalla
ARUSHA : CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimesema kitaendelea kushinda chaguzi zake kwa haki na sio kwa kubebwa.
Akizungumza katika mkutano maalum na viongozi wa CCM Mkoani Arusha, Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa(NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema kuwa CCM inashinda chaguzi zake kwa haki na sio Kwa kubebwa bebwa na itaendelea kushinda kwa sababu wamejipanga vizuri kushinda chaguzi zijazo.
“Hata yule jamaa wa Longido aliyoyasema sio maneno ya Chama mie kama msemaji wa chama niseme yalikuwa maneno yake na ukimsikiliza alikosa hoja huko vichani sijui alifata nini sisi Chama Cha Mapinduzi hatujamtuma na hatuhusiki na maneno sisi tunajipanga kushinda kwa haki na imekuwa kawaida ya kushinda kwa haki,” amesema Makalla.