CCM Tanga yakingia kifua shule za kata

CHAMA Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga kimewataka wananchi kutozibeza shule za kata kwani zimeweza kutoa viongozi ambao wanafanya makubwa katika nchi hii.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Rajab Abdurahman wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Mbugani kata ya Maweni jijini Tanga.

Amesema kuwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ni ushahidi tosha kuwa shule hizo zinaumuhimu mkubwa kwa serikali pamoja na maendeleo ya nchi hii.

SOMA: Nchimbi Katibu Mkuu CCM, Rais ampongeza

“Niwaombe wananchi msipoteshwe na wapinzani ambao wanazisema vibaya shule za kata kwani zimekuwa na mchango mkubwa Kwa nchi hii Kwa zimeweza kutoa viongozi wengi wakubwa ambao wamefanya makubwa katika nchi hii”amesema Mwenyekiti Rajab.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani amesema kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa katika Bandari ya Tanga yamesaidia sasa kupokea meli kubwa za mizigo.

SOMA:Alikua na kazi maalum, CCM imepoteza – Nchimbi

“Tunakwenda kushuhudia meli kubwa nyingine hivi karibu ambayo italeta magari na bidhaa nyingine kutoka nje hivyo hayo ni mapinduzi makubwa Kwa mkoa wetu,”amesema RC Buriani.

Habari Zifananazo

Back to top button