CCM: Vijana msitumike

DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka vijana kutokubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine wasiokuwa na nia njema na nchi badala yake waelewe jukumu lao kubwa katika kulinda amani na usalama wa nchi.

Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ameeleza hayo leo Desemba 6, 2025 katika kikao kazi kilicholenga kuzungumia umuhimu wa amani na usalama nchini.

Akizungumza katika mkutano huo Kihongosi alieleza kuwa vijana wana hatma kubwa na nchi, hivyo hawapaswi kukubali kuichoma nchi au kutumika kwa maslahi ya wengine wasiokuwa na nia njema.

“Tusikubali kuingia kwenye mkumbo utakaogharimu maisha yetu, nawaomba tusiwe sehemu ya vurugu nawaomba vijana msikubali kutumika kwa yasiyistahili kwani pindi yanapotokea matatizo mnabaki wenyewe kuwapa shida wazazi,” alisema Kihongosi.

Aliongeza kuwa vijana hawapaswi kubeba ajenda wasizozijua wala wasikubali kuwa biashara na kukubali kutumika kwa maslahi ya watu, akisisitiza waowashawishi kufanya vurugu wanawaita waliopata madhara yale ni mashujaa wakati wao wamejificha katika mataifa ya watu.

Kihongosi alisisitiza kila mmoja ana jukumu la kulinda amani na kuhakikisha taifa linabaki salama, kwani hakuna atakaye baki salama ikiwa taifa litachafuka, hivyo alisema usalama ni jukumu la kila mtanzania na kulinda amani ni kulinda mustakabali wa taifa.

Katika hatua nyingine, Kihongosi alisema changamoto za ndani ya nchi zitatatuliwa ndani ya taifa, akibainisha kuwa Tanzania ni ni nchi pekee iliyosalama kati ya mataifa yote yanayolizunguka yanashida, hivyo amewataka watanzania kulinde nchi yao na wasiharibu mahali walipozaliwa.

“Tume ya uchunguzi imepewa miezi mitatu itachunguza na kuja na majibu, tuiache ifanye kazi mtu kabka tume haijamaliza kazi yake imeanza tu unaanza kuipinga unaogopa kitu gani,” amesema Kihongosi.

Pia amewataka hatari zinazotokana na mitandao ya kijamii, akibainisha kuwa baadhi ya watu wanatumia mitandao kuhamasisha vurugu, na wengine hushabikia bila kujua madhara yake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka watanzania kuacha ushabiki wa mambo na badala yake wajenge taifa lililo moja kwani huu si muda wa ushabiki, marumbano wala kunyoosheana vidolea.

“Uchaguzi umepita chama kimepita tukae pamoja na kujenga ushirikano kwa mustakabari wa nchi inawezekana kuwa na taasisi ya, dini, chama au taasisis ya elimu yenye mawazo yake wanaruhusiwa kuja kuzungumza na serikali ili tuwezi kujenge,” amesema Chalamila.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button