CCM wapongeza ujenzi Daraja la Magufuli Mwanza

CHAMA  Cha Mapinduzi (CCM), kimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Magufuli lililopo maeneo ya Daraja hilo linalounganisha mikoa ya Mwanza na Geita ujenzi wake umefikia asilimia 51 na linatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2024.

Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amesema chama kinaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wake na ana imani utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa, hivyo mwaka 2024 nchi itakuwa imepata alama kubwa ya kuwa na daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki likiwa na  urefu wa kilomita 3.2.

“Najaribu kukumbuka madaraja mangapi Afrika yenye urefu huo kama hili halitukua la kwanza basi litakuwa katika tatu bora.

“Hivyo niwapongeze wote wanaoshiriki ujenzi wa daraja hili ndugu zetu wa kutoka Korea, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wajenzi kutoka Kampuni ya China na Watanzania wote wanaoshiriki,” amesema Kinana na kuongeza:

“Mnafanya kazi nzuri sana, mnafanya kazi kubwa na Rais (Samia Suluhu Hassan) amenituma nije niwasalimie na niwambie kwamba anangojea aje kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa daraja hili litakapokamilika,” amesema Kinana.

Awali Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa daraja hilo, Abulkarika Majuto,  alisema ujenzi huo kwa sasaa umefikia asilimia 51.

“Tunakukaribisha kwenye ujenzi  wa daraja la JP Magufuli ambalo lina urefu wa kilomita 3.2 pamoja na barabara unganishi za kilomita 1.66,  daraja hili litakapokamilika litaziunganisha wilaya mbili za Sengerema na Misungwi, ambazo zinatenganishwa na Ziwa Victoria kwa kupitia barabara ya  Usagara, Sengerema hadi Geita,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button