Chadema, UDP walichelewa kuwasilisha taarifa za fedha -CAG

DODOMA: MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema katika ukaguzi wake vyama vya siasa viwili vilichelewa kuwasilisha taarifa za fedha kwa makadirio ya kati ya siku 29 hadi 34.
CAG amesema katika taarifa yake kuwa Kifungu cha 18A (2) (a) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 (iliyorekebishwa mwaka 2019) kinataka vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa kuwasilisha taarifa zao za fedha kwa ajili ya ukaguzi ifikapo 30 Septemba 30 kila mwaka.
Amevitaja vyama hivyo kuwa ni Chama cha Kidemokrasia cha Muungano (UDP) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Aidha ameeleza uongozi wa vyama hivyo ulieleza kuwa uchelewaji huo ulitokana na kuchelewa kwa mchakato wa uandaaji wa taarifa za fedha.



