Chalamila amchana mkandarasi Uwanja wa KMC
DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hajaridhishwa na kasi ya mkandarasi anayejenga uwanja wa mpira wa miguu eneo la Mwenge Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Albert Chalamila amesema hayo leo Februari 17,2024 wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ambapo amemtaka Mkandarasi Group six International kabla ya machi 30, 2024 awe amekamilisha ujenzi huo na uwanja uanze kufanya kazi mara moja.
Aidha RC Chalamila amekemea vikali wakandarasi wasio na uwezo na wanachelewesha kazi kuanzia sasa hawatapatiwa kazi zingine katika mkoa huo.
Vilevile RC Chalamila ameelekeza uwanja huo ufanyiwe maboresho ikiwemo sehemu za VIP lakini pia sehemu za kukaa watanzamaji zitengenezwe vizuri zivutue na sio kuweka mbao.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo pamoja na Mstahiki Meya kwa niaba ya madiwani wamesema manispaa hiyo haina mkwamo wowote wa kifedha, fedha zipo changamoto kubwa ni mkandarasi na wao matarajio yao ni kuona awamu ya pili KMC FC wangeanza kutumia uwanja huo.