Chalamila: Hakuna atakayevuruga amani ya Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hakuna mtu y0yote atakayeruhusiwa kuvuruga amani na usalama wa Mkoa huo wala nchi kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa kuhusu hali ya usalama jijini humo, Chalamila amesema kuwa serikali inaendelea kuimarisha ulinzi na kuhakikisha amani ya jiji na taifa inaendelea kudumu.

“Hali ya nchi yetu kwa sasa ni shwari kama alivyoeleza Kamanda Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, na tunaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu, hasa katika kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi,” amesema.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mpango wa biashara masaa 24 jijini Dar es Salaam unaendelea vizuri, na kuwahakikishia wafanyabiashara kuwa wanaweza kuendelea na shughuli zao bila hofu.

“Kwa wale wanaopokea jumbe mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, niwatoe hofu. Endeleeni kufanya kazi zenu kwa amani, hasa kwa wale wanaojihusisha na biashara za usiku,” amesema.

Chalamila pia amewatakia Wakristo maandalizi mema ya sikukuu ya Pasaka, akisisitiza kusherehekea kwa amani na utulivu kama ilivyokuwa wakati wa sikukuu za Idd zilizopita.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button