Changamoto si kigezo cha kutofanya vizuri kwa msanii – Agness Sylvester

DAR ES SALAAM: MSANII chipukizi wa Bongo Fleva, Agness Sylvester maarufu kama Chocolate StarGirl, amesema changamoto zinazowakabili wasanii katika safari ya muziki hazipaswi kuwa sababu ya kukata tamaa au kushindwa kutimiza ndoto zao.
Agness amesema changamoto ni sehemu ya safari ya mafanikio na wasanii wanapaswa kuzitumia kama fursa ya kujifunza, kujenga uzoefu na kuboresha kazi zao badala ya kuzichukulia kama vikwazo visivyoweza kuvuka.
“Changamoto ni kitu cha kawaida kwenye kila sehemu, kwa hiyo mimi nazichukulia kama changamoto na zinanifanya niendelee kufanya vizuri zaidi,” amesema.
Amesema safari yake ya muziki ilianza rasmi mwaka 2021 baada ya kumaliza shule, ingawa mapenzi yake kwa muziki yalianza tangu akiwa mdogo kabla ya kuanza kuimba kanisani na hatimaye kuingia rasmi katika tasnia hiyo.
Kwa mujibu wa Agness, miongoni mwa nyimbo zake za mwanzo ni “Nishakupenda”, huku akieleza kuwa hadi sasa amefikisha jumla ya nyimbo saba.
Akizungumzia kazi yake mpya, msanii huyo amesema wimbo “Wakawaka” umeanza kufanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ya burudani.
Amesema mafanikio ya wimbo huo yamechangiwa na uandishi mzuri pamoja na juhudi za kuutangaza, hali ambayo imewafanya mashabiki kuupokea na kuimba pamoja naye katika maeneo mbalimbali.
Agness amesema kwa sasa hazichukulii changamoto anazokutana nazo kama kikwazo katika safari yake ya muziki, bali anazitumia kama kichocheo cha kuongeza juhudi na kufanya vizuri zaidi.
Amewataka vijana wanaotamani kuingia katika muziki kutokuogopa kuanza, akisema hatua ya kwanza ya kufikia ndoto ni kuwa tayari kuchukua hatua na kuendelea kupambana hata wanapokutana na vikwazo.
Amesema vijana wanapaswa kuamini katika ndoto zao, kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa zinazojitokeza kwa kuwa hakuna anayejua maisha yake ya baadaye yatakuwaje.
Kuhusu maendeleo ya muziki wa Tanzania, Agness amesema tasnia hiyo inaendelea kwenda katika mwelekeo mzuri kutokana na kuongezeka kwa wasanii vijana wanaoibua ubunifu na mitindo mipya.
Amesema anaamini hali hiyo itaendelea kuisogeza mbele tasnia ya muziki nchini na kuongeza ushindani pamoja na ubunifu miongoni mwa wasanii.
Aidha, amewaahidi mashabiki wake kuendelea kuwapatia muziki mzuri na miradi mipya katika kipindi kijacho, akisema anaandaa kazi mbalimbali ambazo anaamini zitawafurahisha na kuwafanya waendelee kufuatilia safari yake ya kisanii.




Everything is very open with a very clear explanation of the issues.
It was really informative. Your site is useful.
Thanks for sharing!
References:
Casino einzahlung sofort https://git.healthathome.com.np/dragonway2