Chicharito:Hersi mfano kwa vijana

DAR ES SALAAM: Chicharito: Hersi mfano kwa vijana UTENDAJI bora, uthubutu na maono imeelezwa kuwa ndio sababu ya vijana wengi kwenye soka kujifunza vitu vingi kutoka kwa Rais wa Yanga, Mhandishi Hersi Said.

Akizungumza na HabariLEO, mtunza vifaa wa klabu hiyo, Godlisten Anderson maarufu ‘Chicharito’ amesema vijana wengi akiwemo yeye wamekuwa wakijifunza masuala mengi kutoka kwa Hersi.

“Ni moja ya watu ambao wanawafanya vijana wengi, wajiamini kwenye uwezo wao, wengi waliamini mpira unaongozwa na wazee, lakini amethibitisha kwa utofauti sana,” amesema Chicharito.

Amesema Hersi amekuwa mfano bora pia kwa viongozi wa soka vijana kwenye timu mbalimbali ndani na nje ya Afrika.

Ikumbukwe November 30, 2023, Rais wa Yanga, Hersi Said alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Shirikisho la Klabu za Afrika (ACA) lenye makao yake makuu yake Nairobi.

Habari Zifananazo

Back to top button