Chokochoko za kisiasa hatari kwa Umoja wa Kitaifa – Shaka

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) amelaani kauli za baadhi ya wafuasi, wanachama na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani Zanzibar zenye kuhubiri mgawanyiko na kuchochea uvunjifu wa amani.

Shaka ameyasema hayo jana Desemba 17, 2022, wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyi yaliyofanyika kisiwani Pemba.

“Chama Cha Mapinduzi kinalaani vikali vitendo vilivyoanza kujitokeza siku za karibuni hasa kisiwani Pemba kwa baadhi ya wafuasi, wanachama na viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa kuhubiri mgawanyiko kuchochea uvunjifu wa amani, sio utamaduni wetu wazanzibari, sio utamaduni wetu Watanzania, CCM inalaani vikali.”Amesema Shaka

Ameema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 Ibara ya 9(a) imeahidi katika kipindi cha miaka mitano kazi kubwa itakayofanywa na CCM ni kuimarisha maridhiano, kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Shaka amesema kazi hiyo inafanywa vizuri na Rais Dk. Samia na Rais Dk. Mwinyi. “Kuweni na amani wana CCM. Hamtajutia kumwani Dk. Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, nia yake ni kutuvusha.”

Shaka amesema Rais Dk. Samia na Rais Dk. Mwinyi ni nyenzo muhimu katika kuendeleza mapatano, maridhiano na masikilizano ya kisiasa nchini.

“Wameanza vizuri sana kwa sababu wana baraka za Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button