Uchumi wa chama ni nguvu ya siasa

GEITA: CHAMA Cha Mapinduzi Kimesema siasa haiwezekani bila kuwa na uchumi imara, kwani nguvu na mafanikio ya chama chochote cha siasa inatokana na uimara wa uchumi wake na ndiyo msingi wa mafanikio ya chama hicho.

Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenan Kihongosi ameeleza hayo leo Aprili 17,2026 alipotembelea mradi wa kitega uchumi wa chama unaojengwa katika eneo la Sabasaba Kata ya Kalangalala Geita Mjini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani Geita.

Akizungumza baada ya kukagua mtadi huo Kijongosi amesema katika mkutano uliopita walikuwa na maazimio 18 na miongoni mwa maazimio hayo kulikuwa na jukumu la kuimarisha uchumi wa chama pamoja na jumuiya zake na geita imetekeleza maazimio hayo kwa vitendo.

“Wapo wanaouliza CCM inawezaje kufanya shughuli zake kwa ufanisi mkubwa, jibu ni rahisi sana tunajenga uchumi wa chama, tunawekeza, tunapata mapato, na mapato hayo yanawezesha shughuli zote za chama kuendeshwa kwa ufanisi,” amesema Kihongosi.

Ameongeza; “Ni ukweli usiopingika siasa bila uchumi haiwezekani na CCM kimeendelea kuwa kinara katika kuhakikisha kinaimarisha uchumi wake, huku kikisimamia pia maendeleo ya wananchi kupitia serikali yake”.

Amesema mradi huo mkubwa unagharimu zaidi ya Sh bilioni tatu, ukiwa na zaidi yavyumba vya biashara 212 na baadhi vimeanza kutoa huduma na zimepata wapangaji, huku nyingine mikataba yake ikiwa imekamilika.

“Chama hiki kinajengwa na wanachama wenyewe, waasisi wetu walifanya kazi kubwa ya kutafuta maeneo, kuyamiliki na kuyaendeleza, leo sisi tunafaidi matunda yao.Hivyo basi, na sisi katika nafasi zetu tuendelee kununua maeneo mapya, kuyakata hati, na kuendeleza miradi ili vizazi vijavyo vikute chama imara kiuchumi,” amesisitiza Kihongosi.

Akisoma taarifa ya mradi huo Katibu wa Chama Wilaya ya Geita, Michael Msuya wameendelea kujenga msingi imara wa kiuchumi latika wilaya hiyo kwa kupitia uwekezaji huo wa kitega uchumi kwa zaidi ya Sh bilioni 3.4.

Akifafanua kuwa mradi huo umegawanywa katika awamu tatu kwanza chama kitapata zaidi ya Sh milioni 12 kwa mwezi ya pili mapato yataongezeka hadi zaidi ya Sh milioni 16 kwa mwezi na ya tatu chama kitapata zaidi ya Sh milioni 24 kila mwezi.

Mwisho.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button