Chongolo awasili Bukombe

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo leo Mei 15, 2023 amewasili wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita kwa ziara ya siku moja.
Katika ziara hiyo atazindua majengo mbalimbali ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwemo ukumbi wa mikutano, nyumba ya kupumzika wageni (Rest House) na mgahawa (Restaurant).
Katibu Mkuu ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Ussi Gavu.