KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewasili wilayani Mlele mkoani Katavi akiendelea na ziara yake ya kukagua uhai wa chama na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya chama kwa Wananchi.
Baada ya kuwasili wilayani hapa leo, Chongolo amesalimiana na chifu wa kabila la Wakonongo, mwenye utawala wa eneo la Kalovya, Chifu Michael Kayamba.
Chongolo ametembelea na kukagua mradi mkubwa wa Bwawa la Nsenkwa, linalojengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji safi na salama kwa matumizi ya Wananchi wa vijiji 16 katika Halmashauri ya Mlele Mkoa wa Katavi.
Mradi huo utawahudumia wananchi 68,000 utagharimu Sh bilioni 2.
8
Akiwa katika eneo hilo la mradi, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo,Chongolo aliwapongeza kwa kubuni jambo litakalokuwa na matokeo makubwa na chanya kwa Wananchi, kwa gharama ndogo.