Chuo cha Utalii kuwanoa Muhimbili

Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), kitaingia kwenye makubaliano na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) yenye lengo la kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wote wa hospitali kwenye masuala ya ukarimu na namna ya kutoa kiwango cha juu cha huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi, wakati wa mazungumzo kati yake na Ofisa Mtendaji Mkuu wa NCT, Dk Florian Mtey, alipotembelea MNH kuona namna ambavyo taasisi hizo zinaweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali.

Prof. Janabi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu Utalii Tiba nchini, amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza sana kwenye sekta ya afya kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa, kanda hadi taifa, lakini bado kuna changamoto ya ukarimu wakati wa kuhudumia wananchi.

“Ni kweli kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na changamoto ya kukosekana ukarimu wakati wa kutoa huduma za matibabu na bado tuko nyuma kama baadhi ya nchi nyingine zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara kama watoa huduma.

“Tunaweza kufanya upasuaji mzuri, tukapandikiza figo, uloto……lakini ile huduma bora kwa mteja tunahitaji kuiboresha.

“Sisi kwetu kama MNH ni jambo lenye afya na bora, hivyo tutashirikiana na NCT kuliboresha ili tuwe na watu wanaoweza kutoa huduma za ziada wanapomhudumia mwananchi, hapo ndio tutaweza kutoa huduma bora na si bora huduma,”amesisitiza Prof. Janabi.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa NCT, Dk Florian Mtey ameipongeza MNH kwa kazi kubwa ya kuhudumia wananchi wa ndani na nje na kuongeza kuwa kuna mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji tangu Prof. Janabi ateuliwe kuisimamia MNH.

Amesema NCT imeona fursa kubwa ya kushirikiana na MNH katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuleta wanafunzi wake kupata mafunzo kwa njia ya vitendo (intership) katika maeneo wanayofundisha ikiwemo, mapokezi, ukarimu na masuala ya kuhudumia wateja.

“Kwa kuanza mashirikiano haya tutaanza kwenye maeneo ya utoaji mafunzo kwa watumishi wote wa MNH hasa kwenye ukarimu na huduma bora kwani sisi tuna weledi na ubobezi kwenye maeneo hayo na pia wanafunzi wetu katika maeneo hayohayo watanufaika na mafunzo kwa njia ya vitendo, ” amesema Dk Mtey.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ruth Prather
Ruth Prather
2 months ago

I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link… 
Try it, you won’t regret it!….. https://workscloud441.pages.dev/

Last edited 2 months ago by Ruth Prather
Theresa J. Evans
Theresa J. Evans
Reply to  Ruth Prather
2 months ago

Make everyone ( $26,000 __ $38,000 ) A Month Online Making money online more than $20k just by doing simple work With No Prior Experience Or Skills Required. Be Your Own Boss And for more info visit any tab this site Thanks a lot just
open this link.======> http://www.pay.hiring9.com

Anna
Anna
2 months ago

Make c4 everyone ( $26,000 __ $38,000 ) A Month Online Making money online more than $20k just by doing simple work With No Prior Experience Or Skills Required. Be Your Own Boss And for more info visit any tab this site Thanks a lot just
open this link.======> http://Www.SalaryApp1.com

Last edited 2 months ago by Anna
Anna
Anna
2 months ago

Make everyone ( $26,000 __ $38,000 ) A c5 Month Online Making money online more than $20k just by doing simple work With No Prior Experience Or Skills Required. Be Your Own Boss And for more info visit any tab this site Thanks a lot just
open this link.======> http://Www.SalaryApp1.com

Last edited 2 months ago by Anna
Eva
Eva
2 months ago

I’m making more than $75k by just doing very easy and simple online job from home.Last month my friend sis received $94280 from this work by just giving only 2 to 3 hrs a day.Everybody start earning money online. visit for more details…
 
 See………..>>  https://Www.Easywork7.com

MelanyDorman
MelanyDorman
Reply to  Eva
2 months ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ https://onlinesite76.blogspot.com

Last edited 2 months ago by MelanyDorman
Back to top button
6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x