Clara Luvanga mfungaji bora Saudi Arabia

JEDDAH, Saudi Arabia: MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania katika soka la wanawake, Clara Luvanga (19) ameibuka kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya Wanawake nchini Saudi Arabia huku akiiwezesha klabu hiyo kutwaa Kombe la Ligi.
Luvanga ameshuka dimbani mara 11 na kufunga mabao 11 katika klabu hiyo aliyojiunga nayo msimu wa 2023/24 akitokea klabu ya LUX Logrono ya Hispania.

Luvanga kabla ya kucheza kimataifa, mwaka 2022 alikuwa akihudumu na klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.