CONGO : WIZARA ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imepanga kutoa taarifa rasmi kuhusu ugonjwa usiojulikana ambao umeua takriban watu 79 katika jimbo la Kwango kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Mpaka sasa zaidi ya watu 300 walioambukizwa walikuwa na. dalili za mafua ikiwemo homa kali, maumivu ya kichwa, mafua pua na kikohozi, ugumu wa kupumua na upungufu wa damu.
Afisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika amesema hivi sasa wametuma timu ya madaktari katika eneo hilo ili waweze kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.
Mamlaka za afya nchini humo zimewataka wakazi kuwa watulivu na waangalifu katika kipindi hiki kigumu huku wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo. SOMA: Ugonjwa usiojulikana wazuka Congo
Pia wametahadharusha wananchi kuzingatia kunawa mikono kwa sabuni, kuepuka mikusanyiko ya watu na kuepuka kugusa miili ya marehemu bila ya kibali cha wahudumu wa afya.