DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Upimaji wa Afya kwa Jamii wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Dk Pedro Pallangyo amewashauri wananchi kunywa maji lita mbili kwa siku ili kukabiliana na hali ya kukaukiwa na maji mwilini.
Akizungumza na Daily News Digital daktari huyo amesema: “Kwasasa ni kipindi cha joto tahadhari za kuchukua ni kuhakikisha kuwa mtu anakunywa vimiminika vya kutosha hasa maji kwamba miili yetu iendelee kufanya kazi kama inavyotakiwa na kutokukaukiwa.”
Ameongeza: “Kiwango cha maji kinachoshauriwa kitaalamu kwa ambao hawana katazo kama wangonjwa wenye tatizo la moyo kufeli ,wagonjwa wenye matatizo ya figo wanashauriwa kunywa maji ya kutosha takribani lita mbili na nusu na kuendelea kwa siku.”
Amesema ili mtu ajue kuwa anatumia maji ya kutosha aangalia rangi ya mkojo wake ambayo inatakiwa kukaribiana na rangi ya maji inavyozidi kuwa haifanani ni kiashiria kuwa unywe maji ya kutosha .
“Joto kali madhara ya kiafya ya moja kwa moja ni kukaukiwa na ukiwa mazingira ya nje unapigwa jua inaweza kuathiri Ngozi,”amesisitiza Dk Pallangyo.