UFARANSA : MAHAKAMA mjini Paris imepanga kutangaza hukumu dhidi ya daktari wa zamani wa Rwanda, Eugène Rwamucyo ambaye anatuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka1994.
Waendesha mashtaka nchini humo wameiomba Mahakama kumfunga miaka 30 jela kwa Eugène Rwamucyo ambaye anatuhumiwa kwa mashtaka ya mauaji ya kiholela, kushiriki na kupanga kufanya uhalifu u dhidi ya binadamu.
Hatahivyo, upande wa utetezi umeendelea kukanusha tuhuma dhidi ya Eugène Rwamucyo,ambaye hakuhusika na mashtaka yanayomkabili.
Mashahibi mbalimbali nchini Rwanda walisafirishwa kwa ajili ya kutoa ushahidi kuhusu mauaji ya kutisha yaliyotokea katika eneo le Butare nchini Rwanda .
SOMA : Ufaransa yasafishwa tuhuma mauaji ya kimbari Rwanda
Hii itakuwa ni kesi ya saba tangu kusomwa na kusikilizwa inayohusiana na mauaji ya halaiki ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994.