Dalai Lama aomba msamaha madai ya kunyonywa ulimi

KIONGOZI wa Kiroho wa Tibet, Dalai Lama ameamua kuomba radhi baada ya picha jongefu kuenea mtandaoni ikionesha akimuuliza mvulana kama anaweza nyonya ulimi wa kiongozi huyo.

Ofisi yake imesema, Lama alitaka kumuomba radhi kijana huyo na familia yake “kwa kile kinachoweza kuwa sababu ya maneno yake.”

Video hiyo pia inaonyesha Dalai Lama akimbusu midomo ya mtoto huyo.

“Lama mara nyingi huwakejeli watu anaokutana nao na kucheza, hata hadharani na mbele ya kamera. Anajutia tukio hilo,” ofisi yake ilisema.

Picha hizo zimezua ukosoaji mkubwa, Shirika la Habari la Uingereza BBC limeripoti.

Kulingana na taarifa hiyo, mvulana huyo alimuuliza Dalai Lama kama angeweza kumkumbatia – hii haionekani katika kipande hicho cha sekunde 23 kinachosambazwa mtandaoni.

Haijabainika ni lini na wapi tukio hilo lilifanyika. Kutoa ulimi nje kunaweza kuwa aina ya salamu huko Tibet.

Dalai Lama amekuwa akiishi uhamishoni nchini India tangu kutoroka Tibet mwaka 1959, kufuatia maasi dhidi ya utawala wa China.

Chanzo: BBC

Habari Zifananazo

Back to top button