Dangote kuzindua kiwanda cha kusafisha mafuta leo

KIWANDA cha Kusafisha Mafuta cha Dangote nchini Nigeria kitaanza kufanya kazi leo Jumatatu Mei 22, mwaka huu huku kukiwa na matumaini ya kukomesha uhaba wa mafuta unaojitokeza mara kwa mara nchini humo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kuzindua kiwanda hicho ambacho kinatarajiwa kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.

Nigeria huaagiza petroli, dizeli na bidhaa za kusindika mafuta kutoka nje kwa sababu mitambo yake ya kusafisha iliharibika miaka mingi iliyopita.

Serikali ya Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari itashuhudia kiwanda hicho kikisafisha mapipa 650,000 kwa siku (bpd).

Habari Zifananazo

Back to top button