Dar kitovu cha mafuta, bei hutegemea soko la dunia

DAR ES SALAAM — Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkoa huo ni kitovu kikuu cha upokeaji wa mafuta nchini Tanzania, ukiwa na matanki 22, kati ya 26 yakijumuisha yaliopo Tanga na Mtwara.

Amesema matanki hayo yana uwezo wa kuhifadhi jumla ya lita 1,346,000, hatua inayosaidia kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini.

Hata hivyo, Chalamila amesisitiza kuwa uwepo wa akiba ya mafuta hauimaanishi moja kwa moja kuwa bei ya mafuta itabaki ile ile.

Akizungumza na waandishi wa habari, alieleza kuwa bei ya mafuta huamuliwa na mambo makuu matatu: bei katika soko la dunia, gharama za uagizaji (premium), pamoja na mabadiliko ya thamani ya fedha za kigeni.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Aliongeza kuwa bei hiyo pia huathiriwa na tozo za kisheria zilizoidhinishwa na Bunge, hivyo kufanya bei ya mafuta kubadilika kulingana na mazingira ya kiuchumi ya ndani na nje ya nchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button