Wafanyabiashara Simu 2000 wapangiwa maeneo ya muda

DAR ES SALAAM — Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema wafanyabiashara wa soko la Simu 2000 Market wamepangiwa maeneo ya muda wakati ujenzi wa maduka zaidi ya 900 ukiendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari, Chalamila alisema zoezi la usafi katika soko hilo tayari limekamilika kufuatia maelekezo ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya biashara na usalama.

Alibainisha kuwa ujenzi wa maduka hayo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu hadi minne, huku serikali ikiendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo.

Aidha, amesema wafanyabiashara wameelekezwa kupanga meza katika maeneo ya muda ili kuendelea na shughuli zao wakati ujenzi ukiendelea.

Chalamila aliongeza kuwa mchakato wa utoaji wa mikopo kwa wafanyabiashara wenye sifa tayari umeanza, ikiwa ni hatua ya kuwawezesha kiuchumi katika kipindi cha mpito.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button