Dar yaomba bajeti Sh bil 992 miradi, mishahara

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkoa huo unaomba kuidhinishiwa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2027 yenye jumla ya Sh bilioni 992 na milioni 601 kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na mishahara ya watumishi.

Akizungumza jana jijini humo katika kikao cha RCC, Chalamila amewashukuru wajumbe kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusimamia na kuendeleza maendeleo ya mkoa huo.

Amesema sekretarieti ya mkoa itakusanya na kuandaa kwa kina hoja na maoni yote yaliyotolewa na wajumbe ili kusaidia katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mkoa.

Katika kikao hicho pia amesisitiza umuhimu wa kuharakisha usajili wa barabara ambazo bado hazipo katika mitandao ya TARURA na TANROADS ili ziingizwe rasmi katika mtandao wa barabara za mkoa.

Amefafanua kuwa hatua hiyo itasaidia kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uboreshaji wa barabara hizo katika miaka ijayo ya fedha.

Aidha, Chalamila ameelekeza kuwa ndani ya wiki moja taarifa za utekelezaji wa miradi ya DMDP kwa kila jimbo ziandaliwe.

Taarifa hizo zinapaswa kuonyesha urefu wa barabara zinazojengwa, bajeti ya mradi, mkandarasi anayetekeleza kazi, kiasi cha fedha kilichotolewa pamoja na asilimia ya utekelezaji wa mradi.

Ameongeza kuwa juhudi hizo zinalenga kuhakikisha maendeleo yanaonekana katika majimbo yote ya mkoa wa Dar es Salaam ili wananchi wote wanufaike na rasilimali za taifa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. This delta 9 sleep gummies felt like a tickety-boo balanced option. It wasn’t too morose and didn’t lean too further in the other direction either, which made it a expert pick for new parts of the day. The finest looked premium, nicely trimmed, and tranquillity wholesome instead of monotonous and crumbly. The flavor came from top to bottom disinfected with a slightly sympathetic and indecent note that made it enjoyable all the path through. Unequivocally a by-product that feels consistent and affectionately send down together.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button