Dar yawaka usajili vijana wenye vipaji

Dar es Salaam iliwaka wakati vijana wenye vipaji mbalimbali walipokutana katika usaili wa Serengeti Lite Nyota Bigi Msimu wa Pili, wakipewa fursa ya kuonyesha uwezo wao na kung’arisha vipaji walivyonavyo.
Usaili huo uliwakutanisha vijana wenye vipaji vya kuimba, kucheza, kuigiza, kuchekesha, uanamitindo pamoja na ubunifu wa aina mbalimbali. Wote walipata nafasi ya kuonyesha kile wanachoweza mbele ya watazamaji na wataalamu wa tasnia.
Kupitia ushirikiano na KUNTA Africa, Serengeti Lite inaendelea kuwawezesha vijana kuamini vipaji vyao, kuvitumia na kufikiria kwa upana zaidi kupitia kaulimbiu “Lite Your Imagination.”
Baada ya Dar es Salaam, safari ya kumtafuta Nyota Bigi inaendelea katika miji ya Arusha, Dodoma na Mwanza, ambako vijana wengine watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuwania nafasi ya kuwa Nyota Bigi wa msimu huu.
Nani ataibuka kuwa Nyota Bigi?
Safari bado inaendelea. Usikose kushuhudia vipaji vikubwa vikichanua!



