DC Bukoba alipa tano shirika mafunzo kwa wanawake

MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima amelishukuru Shirika lisilo la kiserikali la Omuk Hub kwa kutoa ujuzi wa kidigitali kwa kundi la wanawake na vijana ambapo amedai kuwa mafunzo hayo fursa ya kujikomboa kiuchumi kupitia kazi na Biashara wanazozifanya.

Akifungua mafunzo kwa wanawake viongozi wa Mkoa wa Kagera kutoka kwenye vyama vya siasa , yaliyohusu utawala wa taarifa za kiafya yanayoratibiwa na Shirika la Omuk Hub kupitia kampeini ya “Taarifa yangu ya Afya ,Afya Yangu ” alisema kuwa mafunzo ya maswala ya kidigitali yanamsaada mkubwa hasa katika kuhakikisha taarifa za mgonjwa zinazokuwa katika zahanati moja zinakuwepo katika zahanati au vituo vya Afya nchini.

Alisema kuwa serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa mtandao katika maeneo ya vijijini ambapo wananchi wake wanaweza kutumia nafasi ya upatikanaji wa mtandao kutangaza Biashara zao,kufungua kurasa zao mtandaoni za kuuza bidhaa na kununua huku akisema kuwa Baada ya kuimarika kwa mtandao itakuwa rahisi hata Vituo vya Afya na zahanati kuwa na taarifa ya mgonjwa inayoweza kutumika kituo kimoja Hadi kingine.

“Nimekuwa nikishuhudia kazi kubwa ya kutoa Elimu na ujuzi wa kidgtal kwa makundi mbalimbali ya wanawake wajasiliamali na wanawake viongozi katika mkoa wa Kagera ,na Sasa Ni kampeini kuhusu Afya ya Kidgital,Ni kweli kwa Sasa mgonjwa akipewa Rufaa ya kutibiwa analazimika kurudia vipimo upya kitu ambacho Ni Kama usumbufu kwa mgonjwa lakini naamini serikali ikiimarisha upatikanaji wa mtandao katika vijiji vyetu Basi kampeini hii itafanikiwa kwa asilimia 100 na mgonjwa atakuwa anapata taarifa zake na huduma kupitia file lake moja la Siri lililoko mtandaoni” alisema Siima.

Mwanzilishi wa Shirika la Omuk Hub Mbunge wa Viti maalumu kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali Neema Rugangira alisema kuwa lengo la Mafunzo hayo kwa viongozi wanawake ni kuwajengea uwezo wa kufuatilia Taarifa za Afya za wananchi wanaowaongoza ikiwa Ni pamoja na kupaza sauti kwa serikali kuunda mfumo wa kidgtal utakaowezesha wananchi wote kuanzia ngazi ya jamii kupata taarifa pamoja na kuokoa muda pale anapopata Rufaa katika hospital nyingine ili asianze upya wa kurudia vipimo vyake.

“Tumekuwa tukiona mtu akitoka zahanati kwenda kituo Cha Afya au akipatiwa Rufaa katika hospital za kikanda anarudia vipimo upya hata Kama alivipima Zahanati ,Jambo ilo linachukua muda lakini sio tu kurudia vipimo Bali anahamisha na makabulasha ambayo yanaweza kupotea au kuvujisha Siri za mgonjwa lakini mfumo huu wa kidital unaweza kulinda Siri ya mgonjwa”

Meneja wa Shirika la Omuk Hub Dorce Kaijage alisema Shirika Hilo limeendelea kutoa ujuzi wa kidgtal kwa wanawake hasa maswala ya kutangaza Biashara zao mtandaoni ,kutafuta wateja ,kujilinda na udharirishaji ,kufuatilia maswala ya kisiasa pamoja na kutafuta ujuzi mpya kupitia Internet ambapo mikoa iliyoko pembezoni mwa nchi za Tanzania inanufaika na Elimu hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button