MKUU wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Farida Mgomi amesema kuna umuhimu wa kuanzishwa kwa somo la Uzalendo kuanzia ngazi ya elimu ya msingi akiamini itakuwa sababu ya vijana kulipenda taifa lao wakiwa wadogo.
DC Mgomi ametoa kauli hiyo wakati akichangia ukusanyaji wa maoni ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kilichofanyika Ileje mkoani Songwe.
SOMA: Msiwanyweshe pombe watoto- DC Mgomi
Aidha, Mgomi amegusia maeneo mengine kama kilimo, mawasiliano na mahusiano lakini pia dhana ya utawala bora mambo ambayo kimsingi yatakuwa chachu ya maendeleo kuanzia ngazi ya familia na taifa.
Kikao hicho cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo.