DC Mwenda aipongeza Iramba ongezeko bajeti

SINGIDA:MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda ameridhishwa na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa kupitisha bajeti ya makisio ya mapato ya ndani ya kiasi cha Sh bilioni 3.8 ikiwa ni ongezeko la bajeti hiyo ndani ya miaka mitatu iliyopita ya Sh bilioni 1.2.

Mwenda ametoa pongezi hizo katika Baraza Maalumu la Madiwani kupitia na kupitisha makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Advertisement

“Wilaya yetu inayo mafanikio makubwa sana katika utekelezaji wa bajeti zilizopita, tangu nimefika hapa kumekuwa na ongezeko la bajeti yetu na wakati wote tumekuwa tukiitekeleza kwa mafanikio. Tumeikuta bajeti ya Sh bilioni 1.2, leo kwenye baraza hili imepitishwa bajeti ya Sh bilioni 3.8, haya ni mafanikio makubwa sana,” amesema DC Mwenda.

Soma zaidi: DC Mwenda akagua miradi ujenzi wa shule

Katika hatua nyingine Mwenda ametoa pongezi kwa Wilaya ya Iramba kwa kushika nafasi ya 8 ikiwa na asilimia 13 kati ya kati ya halmashauri 10 zilizoongeza ufaulu mtihani wa darasa la saba kitaifa.

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Iramba likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Innocent Msengi limepitisha Makisio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 ya kiasi cha Sh bilioni 38.08.

Bajeti ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 imewasilishwa na Ofisa Mipango, Fadhil Hassan kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa halmashauri.

Soma zaidi: DC Mwenda aongoza kikao tathmini ya lishe Iramba

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imekadiria kukusanya na kutumia Sh bilioni 38.08 ambapo Ruzuku ya mishahara Sh bilioni 21.8, ruzuku ya matumizi mengineyo Sh bilioni 2.06, mapato ya ndani Sh bilioni 3.8, miradi ya maendeleo 5.2 na wahisani, miradi ya maendeleo Sh bilioni 5.08.

Baraza la Madiwani limepongeza waandaaji wa bajeti hiyo kwa kuzingatia vipaumbele mahususi vilivyowekwa kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri wakiamini miradi ya maendeleo itatekelezwa na wananchi watapata huduma stahiki.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *