DC Rungwe akabidhi pikipiki 61

MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amekabidhi pikipiki 61 kwa maofisa ugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha na kuongeza tija sekta ya kilimo.

Akikabidhi pikipiki hizo, Haniu amewagiza watalamu hao wa kilimo kwenda na kushiriki ipasavyo katika usimamizi na uzalishaji wa mazao ya kilimo, ikiwa ni mbinu bora kuongeza kipato cha kaya na lishe kwa jamii.

Ameagiza pikipiki hizo kutumika kwa malengo mahsusi yaliyokusudiwa, ikiwa ni nyenzo sahihi ya kuwafikia wakulima kuanzia ngazi  ya shina, kitongoji hadi kijiji.

“Tahadhari msiende kutumia pikipiki hizi kama bodaboda mtakuwa mnakiuka malengo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wakulima wanapata ushauri wa kitaalamu na kwa wakati,” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Akishukuru kwa niaba ya maafisa ugani, Jenister Munisi  mtaalamu wa kilimo kutoka Kata ya Kinyala amesema wataenda kutekeleza kwa vitendo uzalishaji wa mazao ya  chakula biashara kwa ngazi ya kaya na jamii kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Back to top button