MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekabidhi magari mawili aina ya Prado TX kwa ajili ya wakuu wa wilaya za Temeke na Kinondoni kwa ajili ya usafiri wanapokamilisha majukumu yao ya kiutendaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati alipokabidhi magari hayo Chalamila amesema kuwa usafiri huo utawasaidia viongozi hao kutembelea miradi, lakini pia Uchaguzi wa mwaka huu na mwakani.
“Magari kwa ajiri ya wakuu wa wilaya za Kinondoni na Wilaya ya Temeke Prado TX usajili umekamilika na magari yapo tayari kukabidhiwa gari STN 3471. STN 3470,”
“Magari haya yametolewa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za maendeleo za serikali lakini pia kusaidia kusimamia chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu na Uchaguzi wa mwakani”
“Viongozi walikuwa wakipata changamoto ya usafiri kwa sasa zimetatuliwa na wamepata magari yenye hadhi sio Bora magari kama mnavyojuwa Serikali hainunuagi mtumba Bali inaninua vitu vipya basi haya magari ni mapya kilomita bado hazijasoma,”amesema Chalamila.
Pia ameongeza kuwa viongozi wamekuwa wakilalamikia madereva kuwa wanakimbiza magari wanapokuwa barabarani wanatakiwa kuwathamini ni watu muhimu.
“Nafikiri itafika wakati itawekwa sheria ya Wakuu wa Wilaya kujiendesha wenyewe mkishaenda Dodoma mara mbili tatu wenyewe mtaona madereva wanaumuhimu wao katika kazi zao.
“Mtataka kupewa dereva msiwauzi wala kuwakasirisha wasije peleka gari kichakani halafu wewe unaumia yeye anakimbia kitu ambacho sio kizuri wadhamini ni watu muhimu kwenu.”amesema Chalamila.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa magari hayo aliyowapati na kuahidi kufanyakazi kwa bidii zaidi.
“Awali nilikuwa napata changamoto ya usafiri unaenda kwenye ziara ya kukagua miradi upo njiani gari inaharibika inakulazimu kuacha ziara ila kwa sasa nitakamilisha majukumu yangu kwa wakati.”amesema Mtambule.