De Bruyne kukipiga Ligi Kuu Marekani

Kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne.

KWA mujibu wa tetesi za usajili kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne, 33, anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Marekani(MLS) kucheza katika klabu ya San Diego wakati mkataba wake utakapokwisha Juni 2025.(GiveMeSport)

Eintracht Frankfurt imeweka thamani ya kati ya pauni milioni 41.6 hadi 50 kwa mshambuliaji wa Misri mwenye umri wa miaka 25, Omar Marmoush, ambaye wawakilishi wake wamefanya mazungumzo na Liverpool.(Sky Germany)

SOMA: Tetesi za usajili Ulaya

Advertisement

Mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 25,  anaongoza orodha ya washambuliaji wa kiwango cha juu Arsenal inayopendekeza kuwasajili. (TeamTalk)

Inter Milan inaonesha nia kumsajili kiungo mshambuliaji wa kihispania anayekipiga Athletic Bilbao, Oihan Sancet, 24, ambaye pia amehusishwa na Aston Villa. (Fichajes – in Spanish)

Liverpool na Arsenal zinaongoza kutaka kumsajili Lamine Yamal, 17, wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania.(Miguel Delaney via TeamTalk)