Diamond akerwa wanaomponda Manara

Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’

MSANII Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekerwa na tabia ya baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kumwandama aliyekuwa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara baada ya kuachwa na mkewe Rushayna.

Diamond Platnumz alisema imekuwa kawaida kwa watu wa kwenye mitandao ya kijamii kufurahia matatizo ya wengine, kitu ambacho hakileti picha nzuri bila kuangalia anapitia mazingira gani.

“Kushadadia na tafrija za baadhi ya watu juu ya mtihani huu wa ndoa ya Bugati, unaonesha ni kiasi gani walivyokua na wivu na husda na ndoa zake ambazo zilikuwa mjadala kila uchwao,”

Advertisement

“Utadhani labda wao walizuiwa kuoa ama kuolewa vile, My brother Haji Manara hili nalo litapita kama mengine yalivyo kwenda na kwa ninavyokujua hata presha huna haya ni mambo ya kawaida kwenye maisha,” alisema Diamond.

Alisema kitendo cha ndoa yake kuvunjika kimemuongezea upeo na umaarufu utaongezeka na utakuwa mwendelezo wa kupata dili za matangazo pamoja na kuzungumziwa nchi nzima.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *