WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana leo Oktoba 26,2024 amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa kituo cha utalii cha Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kituo cha utafiti cha Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) inayotekelezwa chini ya mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Dk Chana amejionea maendeleo ya mradi huo ambapo mradi wa ujenzi wa kituo cha utalii wenye thamani ya Sh bilioni 21.4 umefikia asilimia 31 na kituo cha utafiti chenye thamani ya Sh bilioni 1.55 kimefikia asilimia 80.
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 7, 2024 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo na kuelekeza Wakandarasi kusimamia mikataba yao na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Chana yupo Iringa kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.