Dk Ashatu ataka kasi ya utendaji Wizara ya Viwanda

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amewataka Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kuongeza kasi ya kuwahudumia Wananchi hasa wawekezaji wa ndani na Nje ya Nchi kwani Wizara hiyo ndio mhimili wa uchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Dk Kijaji, Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema hayo leo katika ofisi ya Hazina ndogo Mkoani Morogoro alipofungua kikao kazi cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk Hashil   Abdallah ametoa shukrani za pekee kwa Naibu Waziri kuwa sehemu ya kikao kazi hicho ambacho kinaenda kuonesha dira na mwelekeo wa Wizara.

Dk Abdallah amesema kuwa lengo la kuwaleta pamoja wakuu wote wa taasisi zilizo chini ya Wizara ni kujadiliana kwa pamoja namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara nchini na kuja na mkakati madhubuti wa kiutendaji ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita.

Kikao kazi cha Katibu Mkuu kimehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji   Ally Gugu, Wakurugenzi wa Idara kutoka Wizara ya Uwkezaji, Viwanda na Biashara na Wakuu wa Tasisi zilizo chini ya Wizara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x