Dk. Biteko aagiza matumizi sahihi ya fedha za Serikali

GEITA, Bukombe: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewataka watendaji na watumishi nchini kusimamia matumizi sahihi ya fedha za Serikali kwani fedha hizo ndizo zinazotegemewa na watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa Septemba 24, 2023 akiwa wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanyika toka ateuliwe na kuapishwa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Amesema kuwa, chini ya uongozi wa Rais Samia, kila kitu kilichopangwa kufanyika  kinaendelea kufanyika kutokana na fedha anazotoa katika  miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo mradi wa umeme wa Julius Nyerere (MW 2115), ujenzi wa Daraja wa Busisi, ununuzi wa ndege, madarasa, vituo vya afya, utalii na miradhi mingine kadha wa kadha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa Mkoa wa Geita wamemshukuru Mkuu wa nchi kwa kumuamini Dk.Doto Biteko katika nafasi hiyo kubwa na adhimu na kwamba wana imani kuwa ataitendea haki nafasi hiyo kutokana na historia yake ya uchapakazi na uadilifu.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesifu juhudi zilizofanywa na Dk.Biteko wakati akihudumu kama Waziri wa Madini  na kueleza kuwa amesaidia kuinua mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa nchi na ameahidi kuwa ataendeleza misingi hiyo mizuri ikiwemo ya kufanya utafiti wa madini katika eneo lote la nchi ili wachimbaji wachimbe madini kwa uhakika na hivyo kuongeza mapato ya nchi.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Juliaropst
Juliaropst
2 months ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://smartcareer12.blogspot.com/

Last edited 2 months ago by Juliaropst
juliya
juliya
2 months ago

I’m making $90 an hour working from home. I never imagined that it was honest to goodness yet my closest companion is earning 16,000 US dollars a month by working on the connection, that was truly astounding for me, she prescribed for me to attempt it simply. Everybody must try this job now by just using this website… http://Www.Smartwork1.Com

Last edited 2 months ago by juliya
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x