Dk Biteko ashiriki mbio fupi Bukombe

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko leo Oktoba 10 ameungana na wananchi wa Bukombe kwenye mazoezi ya kukimbia mbio fupi za KM 5.
Tukio hilo ni sehemu ya shamrashamra kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwalimu Duniani yatayofanyika wilayani Bukombe, Oktoba 11.
Mbio hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Paskasi Mulagiri.