Dk Biteko atoa maagizo fedha gesi asilia
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametoa maagizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote katika Mkoa wa Lindi na Mtwara kubadilisha maisha ya wananchi kupitia fedha wanazozipata katika miradi ya mafuta na gesi (Service levy) kwenye maeneo
yanayofanyika shughuli hiyo.
Maagizo hayo yametolewa leo wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji eneo la ugunduzi wa gesi la Ntorya lililopo kata ya Nanguruwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.
Amewataka wakurugenzi hao kukaa kwenye mabaraza yao na kwamba lazima sehemu ya fedha hiyo inayolipwa kupitia kampuni zinazoshughulika na gesi asilia.
“Wakurugenzi muone wivu watu wenu kule wapate hizp huduma kutokea na service levy wakati tunatafuta fedha za CSR wapate na ela ya service levy kwenye maeneo yao tunataka haya maeneo yabadilike haraka, na hili jambo lianze sasa na kama alianzi sasa lianze sas hivi,” amesema Biteko
“Hao wananchi waliyoko huko utulivu wao ndio unatufanya sisi tupate hiyo gesi nataka tuende tukabadilishe maishe yao kupitia fedha tunazozipata”
Akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame amesema visima viwili vimechimbwa katika kitalu hicho katika Ntorya -1 na Ntorya -2 mwaka 2012 na mwaka 2017.
Amesema hadi sasa jumla ya futi za ujazo bilioni 1,642 za gesi asilia zimegunduliwa na kuhakikiwa na leseni hiyo inayotolewa itawezesha gesi hiyo iliyogunduliwa katika kitalu hicho kuzalishwa na kuwezesha kuongezeka kwa kiasi cha gesi kinachozalishwa nchini.
Mradi huo unategemea kuzalisha kiasi cha kuanzia futi za ujazo milioni 60 kwa siku na kuongezeka hadi kufikia futi za ujazo milioni 140 kwa siku katika kipindi cha miaka mitatu.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Shamsia Mtamba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kutekeleza miradi hiyo ya Gesi Asilia kwenye mkoa wao huku akiomba suala la ajira wapewe kipaumbeke wakazi wa maeneo yanayotekelezwa mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kilumbe Ng’enda ametoa pongezi kwa Tpdc kwa kazi kubwa inayofanya katika utekelezaji wa mradi hiyo mafuta na gesi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ARA ya uendelezaji wa kitalu hicho cha Ntorya Erhan Saygi amesema mradi huo utakamilika mwaka 2025 na utaongeza ajira kwa watanzania kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alisema Mkoa huo umepata umeme kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha kutumia Gesi Asilia cha ‘power plant’ ambapo kwa sasa kituo kina mashine 13 zenye uwezo wa kuzalisha mewagati 30.4