Dk Chana afungua shule ya msingi Namlangwa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amefungua shule ya Msingi Namlangwa iliyojengwa kwa Sh milioni 638.5, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa leo Oktoba 1.

Ujenzi wa mradi huo umejumuisha vyumba viwili vya elimu ya awali, vyumba 14 vya elimu Msingi, matundu 24 ya vyoo na kichomea taka.

Advertisement

Akizungumza baada ya kufungua shule hiyo, Dk Chana ametoa rai kwa maofisa elimu na serikali za vijiji kufuatilia takwimu za wanafunzi wanaopaswa kwenda shule na kuwarejesha ambao hawako shule.

SOMA: Dk Chana afungua sekondari Josephat Kandege

“Urithi pekee unaoweza kumpa mtoto ni elimu, tunataka taifa ambalo limeelimika na lenye nguvu kazi ya kutosha,” amesema Dk Chana.

Amesema aerikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha Watanzania wanapata elimu bure na bora.

Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mkuu wa Shule ya Msingi Namlangwa, Enock Elly ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha za mradi wa BOOST ambazo zimesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuongeza ufanisi wa walimu katika kutelekeza majukumu yao.

1 comments

Comments are closed.