Dk Chana afungua sekondari Josephat Kandege
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amefungua shule mpya ya Sekondari ya Josephat Kandege, Kata ya Mpombwe,Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa leo Oktoba 1,2024.
Shule hiyo ya kutwa ya Serikali yenye mchanganyiko wa wasichana na vavulana imegharimu Sh milioni 583.1 ambapo yamejengwa madarasa manane, jengo la Tehama, maabara ya kemia na bailojia, maabara ya fizikia, jengo la utawala, vyoo vya wanafunzi na tanki la maji.
SOMA: Dk Chana ataka ubunifu TFS
Akizungumza mara baada ya kuifungua shule hiyo, Dk Chana amesema fedha za ujenzi wa shule hiyo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Ametumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kuhakikisha watoto wao wanaenda shule kwani elimu ni ufunguo wa maisha.
Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Josephat Kandege, Talian Bahati amesema mafanikio yaliyopatikana ni kutoa ajira kwa wananchi na kusogeza elimu kwa wanafunzi waliokuwa wanatembea umbali zaidi ya kilomita 20.
2 Comments