RUKWA: WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana ametembelea shamba la Miti Mbizi, ambalo liko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa kukagua uendelevu wa chanzo cha maji cha Mbizi na kuona mchango wa shamba kwa jamii.
Katika ziara hiyo, Dk Chana aliongozana na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile pamoja na wahifadhi kutoka shamba la Miti Mbizi.
Comments are closed.