Dk Chana aonya wawekezaji wasioendeleza maeneo

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi, Dk Pindi Chana amesema  wawekezaji waliochukua maeneo mbalimbali na kutoyaendeleza wanakwamisha shughuli maendeleo.

Dk Chana amesema hayo leo alipotembelea Hifadhi ya Taifa Katavi ambapo amesema kushindwa kufanya uwekezaji ndani ya makubaliano kunasababisha ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na kuikosesha mapato ya serikali.

Advertisement

Waziri Dk Chana amezielekeza halmashauri zote nchini kuweka ajenda ya kudumu ya uhifadhi wa misitu na mazingira katika vikao vya serikali za vijiji ili kuona namna gani kila kijiji kimejiwekea mikakati ya kuzuia na kudhibiti masuala ya moto.

SOMA: Dk Chana akagua chanzo cha maji Miti Mbizi

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi mkoani Katavi, Abel Mtui amesema hifadhi hiyo ni mashuhuri yenye vivutio vingi na wanyama adimu ambapo pia inasikifika kuwa na idadi kubwa ya viboko.

Hifadhi ya Taifa Katavi ina ukubwa wa kilomita za mraba 4,471 ambayo ni kati ya hifadhi kubwa 500 za taifa ikitanguliwa na hifadhi ya Nyerere, Ruaha, Serengeti na Burigi Chato.