Dk Mpango akutana na Katibu Mkuu UN

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Guterres yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika jijini Nice nchini Ufaransa leo Juni 10, 2025.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa kupitia Taasisi mbalimbali zilizo chini ya umoja huo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)