Ushirikiano mpya wafungua fursa za masoko

DAR ES SALAAM:SHIRIKISHO la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) limesaini rasmi Hati ya Makubaliano (MoU) na Kituo cha Taifa cha Kukuza Mauzo ya Nje (NEPC) cha Jamhuri ya Belarus, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam Rais wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula wakati wa utiaji saini uliofanyika katika ziara rasmi ya Maxim Ryzhenkov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus, aliyeambatana na Balozi Nikolai Borisevich, Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kukuza Mauzo ya Nje cha Belarus (NEPC).

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mahmoud Thabit Kombo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, na Dk, Bashiru Ally Kakurwa ( Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ikionesha ushirikiano imara kati ya Serikali na sekta binafsi.

Katika hatua nyingine Angelina amesema MoU hii inaweka mfumo wa kuimarisha mauzo ya nje, kukuza ushirikiano wa kibiashara, na kutekeleza mipango ya pamoja, ikiwemo maandalizi ya Jukwaa la Biashara la Tanzania -Belarus, linalotarajiwa kufanyika wakati wa ziara rasmi ya Alexander Turchin, Waziri Mkuu wa Belarus baadaye mwaka 2026.

Aidha, Angelina amesema TPSF itaendelea kujizatiti katika kuendeleza ushirikiano wa kimataifa unaofungua fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania na kuimarisha ushiriki katika biashara za kimataifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button