Mwigulu:Mafanikio AFCON yameitambulisha zaidi Tanzania

DODOMA; WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, ameipongeza timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufikia hatua ya 16 bora fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2025 zilizomalizika mwezi uliopita nchini Morocco na kwamba mafanikio hayo yameitambulisha zaidi Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Februari 6, 2026 kwenye hotuba yake ya kuahirisha shughuli za Bunge la 13 Mkutano wa Pili ulioanza Januari 27, 2026.

“Nitumie fursa hii adhimu kuipongeza Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) kwa kufanikiwa kuandika historia kwa kufuzu hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

“Tangu kuanzishwa mashindano haya, Tanzania imefanikiwa kushiriki mara nne, mwaka 1980 nchini Nigeria; mwaka 2019 nchini Misri; mwaka 2023 nchini Ivory Coast na mwaka 2025 nchini Morocco ambapo tumeweka rekodi ya kuingia 16 bora.

“Mashindano ya AFCON hutazamwa na watu wengi duniani, hivyo, mafanikio haya yameiwezesha Tanzania kutambulika zaidi katika ramani ya soka barani Afrika na duniani kote,” amesema Dk Nchemba.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button