Dk.Mwinyi azindua Chuo cha Ualimu Nkrumah

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha maslahi ya walimu ili kuwaongezea motisha na mazingira bora ya kufundishia.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 14 Agosti 2025, baada ya kuzindua rasmi Chuo cha Ualimu cha Nkrumah kilichopo Mfenesini, Mkoa wa Mjini Magharibi. SOMA: Mradi wa OCP School Lab wanoga ZanzibarAmeeleza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati na mikakati ya kuimarisha sekta ya elimu ili mafanikio yanayopatikana sasa ya ongezeko la ufaulu wa wanafunzi katika ngazi mbalimbali yawe ya kudumu.

Rais Dk. Mwinyi amefahamisha kuwa azma ya kukirejesha chuo hicho, ambacho kilikuwa chimbuko la umahiri na uandaaji wa walimu bora.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button