Dk Ndumbaro ateua bodi BAKITA

Mwenyekiti wa Bodi ya BAKITA, Prof. Martin Mhando.

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro ametangaza Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) yenye wajumbe saba kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa Sheria na Miongozo mbalimbali ya Serikali.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini imesema Mwenyekiti wa Bodi hiyo aliyeteuliwa ni Prof. Martin Mhando.

SOMA: EAC yatenga mamilioni ya fedha kukuza Kiswahili

Advertisement

Wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa ni Francis William Kayichile, Dk. Victor Elia, Dk. Mwanahija Ali Juma, Ivan Ben Tarimo, Dk. Jabhera Matogoro na Nyakaho Mturi Mahemba.

Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho ya mwaka 1983 na 2016, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ana dhamana ya kuteua wajumbe wa Bodi ya BAKITA na kumtangaza Mwenyekiti wa Bodi hiyo.