Dk Possi aonya uchafuzi wa mazingira majini

NAIBU Katibu Mkuu Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Dk Ally Possi, amesema uchafuzi wa mazingira majini una athari za kuzalisha viumbe hatarishi, ambavyo vitakuwa hatarishi kwa mazingira na viumbe vya majini.

Dk Possi amesema hayo wakati wa kongamano la uchafuzi wa mazingira unaotokana na vyombo vya majini hususan meli, lililoandaliwa na Shirika la Bahari Duniani, na kuratibiwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac), jijini Dar es Salaam.

Amesema  Tanzania ina wajibu wa kuhakikisha mazingira majini na vyombo vya usafiri majini havichafui bahari, maziwa na mito kwa sababu ya utunzaji wa mazingira katika maji.

Advertisement

” Mkutano una umuhimu wa kuzingatia makubaliano ya itifaki ambayo ilipitishwa 2004 ikaanza kutumika 2017. Tanzania ni mmoja wa wanachana wa jumuiya hiyo ya kimataifa,” almesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tasac, Kaimu Mkeyenge amesema suala hilo la kuhakikisha mazingira ya bahari yanatunzwa kwa sababu ya kuhakikisha viumbe vitakavyozaliwa siku za mbeleni, dunia imeanza kulipa kipaumbele.

” Vyanzo vya maji vinasimamia sera za uchumi wa buluu na bahari inapochafuka au kuharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa buluu inakuwa ngumu kwa sababu viumbe vinavyofanya uchumi kama samaki hupotea, pia mazingira huharibika na kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa ” amesema.

 

Alisema baada ya kongamano hilo wadau watakuwa na uelewa mpana wa jambo hilo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *