Dodoma Jiji kulamba asali Ligi Kuu leo?
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa mkoani Dodoma.
Wenyeji Dodoma Jiji itaikaribisha Tabora United kwenye uwanja wa Jamhuri.
SOMA: Kivumbi ‘derby’ ya majiji Ligi Kuu leo
Mchezo uliopita kwenye uwanja wa Jamhuri , Dodoma Jiji ilipoteza mbele ya Simba kwa bao 1-0.
Dodoma Jiji inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 6 ikishinda mechi 1, sare 3 na kupoteza 2.
Tabora United ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 8 baaa ya michezo 6 ikishinda 2, sare 2 na kupoteza 2.
Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu timu hizo kukutana Machi 6,2024, Dodoma Jiji ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Tabora United.