Dola milioni 1.94 kulinda maji Wami – Ruvu

KAMPUNI ya Coca-Cola Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) na Serikali kupitia Bodi ya Maji ya Bonde la Wami-Ruvu imezindua mradi wa zaidi ya Dola milioni 1.94 zitakazotumika kurejesha vyanzo vya maji katika kidakio cha Ngerengere mkoani Morogoro.

Mradi huo unaojulikana kama Uhifadhi wa Vyanzo vya maji kidakio cha Ngerengere (NBS4WATER ) ,unalenga kurejesha mazingira, kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji na kuboresha maisha ya wananchi wanaozunguka bonde hilo.

Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza (Tanzania),David Chait amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kidakio cha Ngerengere ulioenda sambamba na upandaji miti kando ya Bwawa la Mindu , mjini Morogoro.

Chait amesema kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza upatikanaji wa maji salama kwa jamii katika eneo la mradi unakotekelezwa ikiwemo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema  kuwa mradi huo ni sehemu ya mpango Coca- Cola Africa Water Stewardship Initiative ulioanzishwa mwaka 2024 na kutekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne .

“ Bonde la Wami-Ruvu ni muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo kuna haja ya kulinda vyanzo vyake” amesema  Chait.

Naye Meneja wa mradi kutoka IUCN, Doyi Mazenzele amesema  zaidi ya wakulima 2,000 watanufaika kwa kufundishwa kilimo kinachokabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema , IUCN ina shirikiana na Serikali kupitia Bonde la Wami – Ruvu  katika kukabiliana na changamoto zinazokabili mto Ngerengere kutokana na ukataji miti, kilimo holela , ufugaji holela , uchafunzi wa maji , na mabadiliko ya tabianchi.

Meneja wa Mradi huyo amesema   mradi unalenga kurejesha maeneo yaliyoathiriwa zaidi ya hekta 3,000 za ardhi kwa kupanda miti ya matunda , miti ya viungo na ufugaji wa nyuki na Samaki ili kujiongezea kipato huku matarajio kuzalisha lita milioni 548 za maji mwisho wa mradi huo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Wami-Ruvu, Juvenalis Tarimo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kulinda rasilimali za misitu na uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mto Ngerengere .

Kwa upande wake  Katibu Mkuu Wizara ya Maji, katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara hiyo, Rosemary Rwegubisa amesema  Serikali imepiga marufuku shughuli zote za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. S­­t­­a­­r­­t m­­a­­k­­i­­n­­g c­­a­­s­­h r­­i­­g­­h­­t n­­­­ow­­… G­­e­­t m­­o­­r­­e t­­i­­m­­e w­­i­­t­­h y­­o­­­­u­­r f­­a­­m­­i­­l­­y b­­y d­­o­­i­­n­­g j­­o­­b­­s t­­h­­a­­t o­­n­­l­­y r­­e­­q­­u­­i­­r­­e ­­f­­o­­r y­­o­­u­­ t­­o ­­h­­a­­v­­e a c­­o­­m­­p­­u­­t­­e­­r a­­n­­d a­­n i­­n­­t­­e­­r­­n­­e­­t a­­c­­c­­e­­ss ­­­­a­­n­­­­d ­­y­­o­­u ­­c­­a­­n h­­a­­v­­e t­­h­­­­a­­t ­­a­­t y­­o­­u­­r h­­o­­m­­e. S­­t­­a­­rvt b­­r­­i­­n­­g­­i­­n­­g ­­u­­p t­­o $­­18­­0­­1­­2 ­­a m­­o­­n­­t­­h. I’v­­e s­­t­­a­­r­­t­­e­­d t­­h­­i­­s j­­o­­b a­­n­­d I’v­­e n­­e­­v­­e­­r b­­e­­e­­n h­­a­­p­­p­­i­­e­­r a­­n­­d­­ n­­o­­w I a­­m s­­h­­a­­r­­i­­n­­g i­­t w­­i­­t­­h y­­o­­u, s­­o­­ yo­­u c­­a­­n t­­r­­y i­­t t­­o­­o. Y­­o­­u c­­a­­n c­­h­­e­­ck i­­t ou­­t h­­er­­e…

    HERE→→→→→ https://PayAtHome1.Com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button