Dorothy Semu kugombea urais 2025

DAR ES SALAAM: KIONGOZI wa Chama cha ACT –Wazalendo, Dorothy Semu ametangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Januari 16, 2025, Dorothy amesema hatua hiyo imesukumwa na mambo manne ambayo ameyaona kama mapungufu.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni, kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, changamoto ya ajira kwa vijana na udhaifu katika usimamizi wa rasilimali za taifa.

“Nimejipima na nimeona ninatosha, nimekuwa kiongozi kwenye nafasi mbalimbali hata kabla ya kuingia kwenye siasa, pia ni kiongozi wa chama bora, chenye sera na ilani bora,” amesema Semu.

Habari Zifananazo

Back to top button